Friday , 3rd Sep , 2021

Mbunge wa kuteuliwa Humphrey Polepole, amesema kuwa kikao cha maadili ni kikao cha ndani hivyo taarifa zote zitatolewa kwa utaratibu wa chama na sio yeye.

Mbunge wa kuteuliwa Humphrey Polepole

Kauli hiyo ameitoa hii leo Septemba 3, 2021, Jijini Dodoma, wakati alipoitikia wito wa Kamati ya Maadili ya Wabunge wa Chama cha Mapinduzi (CCM), ambayo imemuita lakini haikubainishwa wazi sababu zilizopelekea Mbunge huyo kuitwa mbele ya kamati hiyo.

"Kikao cha maadili ni kikao cha ndani, kwahiyo taarifa zote zitatoka kwa utaratibu wa chama," amesema Mbunge Polepole.

Wabunge wengine walioitwa kufika mbele ya kamati hiyo ni Mbunge wa Ukonga Jerry Silaa na Mbunge wa Kawe Askofu Josephat Gwajima.