Friday , 3rd Sep , 2021

Hatimaye familia ya marehemu Wilson Ogeta, wakazi wa Kijiji cha Nyambogo, wilayani Rorya mkoani Mara imeamua kuuzika mwili wa ndugu yao huyo mara baada ya kukaa mochwari kwa muda wa miezi 8 baada ya familia hiyo hapo awali kugoma kuuzika kutokana na mgogoro wa ardhi.

Jeneza lililobeba mwili wa marehemu Wilson Ogeta

Wakizungumza na EATV familia ya marehemu wameiomba serikali kuangalia namna ya kurejeshewa eneo lao ambalo lilichukuliwa kinyume na utaratibu.

Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Rorya Juma Chikoka, alishiriki katika mazishi hayo amewataka wananchi kuwa wavumilivu katika kipinid hiki na wakati serikali ikishughulikia jambo hilo.

Tazama video hapa chini