Naomi Osaka (pichani) muda mchache kabla ya kukutana na kipigo na kuvuliwa ubingwa wa US Open.
Osaka ameondoshwa mashindanoni katika mzunguko wa tatu wa mashindano hayo chipukizi mwennye umri wa miaka 18, Leylah Fernandez.
''Kwakweli sifahamu ni lini nitacheza tena ,nafikiri nahitaji kupata mapumziko ya kutosha ,kwasiku za hivi karibuni hata nikishinda sijisikii furaha, na hata nikipoteza najisikia vibaya, nadhani hali hii sio ya kawaida''alisema Osaka baada ya kupoteza mchezo.
Raia huyo wa Japan alijiamua kujiweka kando na hakushiriki katika michuano ya wazi ya Ufaransa(French Open) kwa maelezo kuwa alikuwa anapambana na matatizo ya afya ya akili tangu atwae grand slam yake ya kwanza mwaka 2018.
Vilevile hakushiriki katika mashindano ya Wimbledon kabla ya kurejea uwanjani katika Olimpiki yaliyofanyika nchini Japan mwaka huu.