Sunday , 5th Sep , 2021

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amewasili mkoani Kilimanjaro kwa ajili ya kuendelea kurekodi kipindi maarufu ya Royal Tour leo Septemba 5, 2021.

Rais Samia Suluhu Hassan katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA).

Rais Samia amewasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa Kilimanjaro (KIA) asubuhi na kupokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Stephen Kagaigai pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Manyara Makongoro Nyerere.

Akiwa Kilimanjaro, Rais Samia ataendelea na zoezi la kurekodi kipindi maarufu ya Royal Tour, ambacho kitarushwa nchini Marekani ikiwa ni sehemu ya kuitangaza nchi pamoja na utalii kimataifa ili kuvutia watalii wengi kuja nchini.

Rais Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Stephen Kagaigai pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Manyara Makongoro Nyerere mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA).

Ndani ya wiki hii, tayari Rais Samia amesharekodi katika maeneo mbalimbali ikiwemo Bagamoyo mkoani Pwani.