Thursday , 23rd Sep , 2021

Bingwa wa zamani wa mkanda wa uzito wa kati wa WBA Welter Weight, Manny Pacquiao amesema kwa sasa inatosha kwa maana ya kutaka kuachana na mchezo huo aliutumikia kwa kipindi kirefu.

Bondia Manny Pacquiao (kulia) akizipiga na bondia Yordenis Ugas wa Cuba kwenye pambano la kuwania Mkanda wa Ubingwa wa Uzito wa kati WBA pambano lililofanyika Agosti 2021 ambapo Pacquiao alipoteza mchezo huo.

Kauli ya Pacquiao mwenye miaka 42 inakuja baada ya familia ya bondia huyo kumtaka astaafu haraka.

"Kazi yangu ya ndondi tayari imekwisha. Imefanywa kwasababu nimekuwabkwenye ndondi kwa muda mrefu na familia yangu inasema kuwa inatosha" 

Kwa upande mwingine, Promota wa Pacquiao, Sean Gibbons amesema bondia wake bado haja staafu rasmi ila anatazamia kupata jibu kmaili siku chache zajazo.

"Seneta ni mgombea wa urais na bado hajafanya uamuzi wowote juu ya maisha yake ya ndondi. Katika wiki chache zijazo atafanya uamuzi wa mwisho ikiwa atakuwa na zaidi au atastaafu" Alisema Sean Gibbons Promota wa Pacquiao.

Pacquiao aliyetangaza nia ya kugombea Urais wa Ufilipino kwenye Uchaguzi mkuu wa mwaka 2022, akitangaza kustaafu masumbwi basi pambano lake dhidi ya Yordenis Ugas wa Cuba mwezi uliopita mwaka huu ambapo Pacquiao alipigwa na kushindwa kuutetea mkana wa WBO.