Thursday , 23rd Sep , 2021

Baada ya teknolojia ya kufunga mfumo wa kutumia gesi asilia kwenye magari kuanza kutumika duniani kumeweza kutoa faida nyingi za kiuchumi na mazingira kwa watumiaji ukilinganisha na nishati ya mafuta.

Magari yanayotumia gesi asilia (NGVs) imesaidia kuboresha hali ya hewa, kuokoa  gharama karibu zaidi ya nusu ya ile ya mafuta ya petroli, kupungua uzalishaji wa gesi chafu, kelele, harufu kidogo na kuleta unafuu katika sekta ya usafirishaji.

Takwimu zinaonyesha kuwa magari  zaidi ya milioni 11 duniani yanatumia gesi asilia na nchi inayoongoza ni Pakistan yenye magari milioni 2.1, Argentina magari milioni 1.8 na Brazil magari milioni 1.7.