Friday , 24th Sep , 2021

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, amesema kuwa ameihakikishia dunia kuwa Tanzania ni ile ile yenye amani na ushirikiano kwa nchi zote.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan

Kauli hiyo ameitoa kupitia ukurasa wake wa Twitter mara baada ya usiku wa kuamkia leo Septemba 24, 2021, kuhutubia Mkutano wa 76 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa.

"Nimehutubia kwa mara ya kwanza Mkutano wa 76 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, nimeihakikishia dunia kuwa Tanzania ni ile ile yenye amani na ushirikiano na nchi zote, nimeeleza imani yangu kuwa changamoto za dunia tunaweza kuzikabili kwa pamoja ikiwemo janga la Uviko-19," ameandika Rais Samia.