Saturday , 25th Sep , 2021

Shule ya Msingi Kisaula iliyopo Kijiji cha Mbongo, Kata ya Manda wilayani Ludewa mkoani Ruvuma inahitaji ufumbuzi wa haraka kwani inakabiliwa na changamoto ya vyoo bora, uchakavu wa vyumba vya madarasa, nyumba za walimu na huduma ya maji katika shule ya hiyo.

Moja ya choo kinachotumiwa na wanafunzi wa Shule ya Msingi Kisaula

Shule ya Msingi Kisaula ina wanafunzi zaidi ya 130 ikiwa haina wanafunzi wa darasa la pili na darasa la nne kutokana na uhaba wa watoto wa kujiunga na madarasa hayo pindi walipokuwa wanaandikisha kuanza mikondo hiyo ya madarasa. 

Kutokana na kuwepo kwa changamoto lukuki zinazoikabili shule hiyo wanafunzi wanalazimika kutumia vyoo vya asili kwa ajili ya haja ndogo na vingine kwa ajili ya haja kubwa, kutokana na kutokuwepo kwa vyoo bora shuleni hapo ambapo pia walimu nao wanalazimika kukaa nyumba moja jinsia tofauti.