Friday , 29th Oct , 2021

Vinara wa NBC Tanzania Premier Ligi, Yanga inataraji kukipiga dhidi ya Azam Jumamosi ya kesho saa 1:00 usiku  Oktoba 30, 2021 kwenye dimba la Benjamin Mkapa bila ya nyota wake wanne kwa sababu mbali mbali.

Yassin Mustapha (Kushoto), Paul Godfrey (katikati) na Dickson Ambundo (kulia).

Nyota hao ni, Mlinzi wa kulia Paul Godfrey ‘boxer’ aliyefiwa na baba yake hivi karibuni ilhali Mlinzi wa kushoto Yassin Mustapha licha ya kucheza kwa dakika 45 mchezo wakirafiki dhidi ya Ruvu Shooting lakini bado hana utimamu kamili.

Winga Dickson Ambundo ameruhusiwa kwenye kuugulia nyumbani kwao kutokana na kufungwa bandeji ngumu kwenye mkono wake alioumia kwenye mchezo dhidi ya Ruvu Shooting wiki iliyopita.

Mchezaji  mwengine anayetazamiwa kukosekana ni kiungo  Mapinduzi Balama ambaye amepona majeraha yake ya mguu lakini anaendelea na mazoezi mepesi ili arejee kwenye utimamu kamili.

Wakati Afisa Habari wa Yanga, Hassan Bumbuli akiithibitishia EA Radio kukosekana kwa wachezaji hao, nae kocha msaidizi wa Yanga, Cedric Kaaze amesema kila mchezo watakuwa wanawakosa wachezaji wawili wa kimataifa kutokana na taratibu za Ligi kuruhusu wachezaji 12 tu wakigeni, wachezaji ambao hakuwaweka wazi.