Sunday , 31st Oct , 2021

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi amesema wizara hiyo haitaruhusu mtu mmoja anunue nyumba nyingi kisha yeye kuzipangisha kwa wengine.

Waziri Mkuu (aliyesimama), Mkuu wa Mkoa wa Dodoma (kushoto waliokaa) na Waziri wa Ardhi William Lukuvi (kulia)

Waziri Lukuvi amezungumza hayo katika uwekaji wa jiwe la msingi katika mradi wa nyumba 1000 kwenye nyumba za makazi zilizopo eneo la Chamwino na Iyumbi jijini Dodoma.

"Hatutakubali mtu aje anunue nyumba 300 halafu yeye ndio ageuke shirika la nyumba kwa kupangisha watu, hilo haliwezekani," amesema.

Sehemu ya nyumba hizo

Aidha Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ambaye alikuwa mgeni rasmi alisema mradi mkubwa unaohusisha ujenzi wa nyumba za makazi 1000 katika Jiji la Dodoma utagharimu Shilingi bil. 71 hadi kukamilika. 

Awamu ya kwanza yenye nyumba 404 itagharimu shilingi bilioni 21.4 na kazi kubwa ya ujenzi itakuwa imekalika ifikapo Desemba 2021.