Makamu Mwenyekiti wa chama cha ACT Wazalendo Zanzibar, Juma Duni Haji
Taarifa hiyo imetolewa leo Novemba Mosi, 2021, na Naibu Katibu wa Habari wa chama hicho Janeth Rithe, na kusema kuwa Duni aliandika barua yake ya kujiuzulu nafasi yake ya Makamu Mwenyekiti mnamo Oktoba 30, mwaka huu.
Uchaguzi wa Mwenyekiti wa chama, Makamu Mwenyekiti wa Zanzibar na uchaguzi wa nafasi moja ya Mjumbe wa Halmashauri Kuu Taifa, utafanyika Januari 29, 2022.







