Friday , 19th Nov , 2021

Espanyol wanataraji kuwa wageni wa Barcelona kwenye derby ya Catulanya itakayochezwa Jumamosi ya November 20, 2021 katika dimba la Nou Camp. Kuelekea kwenye mchezo huo shabiki wa Espanyol, Ramon Orriols amesema kuwa watani wao walitamani kuwaona wakipotea kwenye ramani ya soka.

(RCD Espanyol de Barcelona)

“Nadhani mashabiki wa Barcelona walitaka tushuke na kutoweka kabisa kwenye ramani ya soka. Hawatupendi na wanataka kuwa watawala wa soka la Kikatalani. Hilo lilikuwa jambo gumu. Nashukuru hakukuwa na mashabiki uwanjani kutokana na janga la Corona” anasema Ramon Orriols, ambaye sasa anaishi Uingereza na ni sehemu ya wafuasi wa klabu ya Espanyol.

Kwa takriban miaka 80 mashabiki wa Espanyol wamelazimika kukubali kumaliza chini ya Barcelona kwenye ligi kuu ya Hispania huku wakitamani kuishi kwenye daraja moja la Cules.

Ziara yao ya mwisho kwenye dimba la Nou Camp ilikuwa ni siku chungu katika historia ya Espanyol baadaya Luis Suarez kufunga katika ushindi wa 1-0 kwa wenyeji Julai mwaka jana na kuthibitisha Espanyol kushuka hadi daraja la kwanza kwa mara ya kwanza tangu kampeni za 1993-94.

Nico Melamed, mmoja wa nyota wachanga wanaotegemewa sana wa Espanyol, alikuwa mchezaji wa akiba ambaye hakutumiwa siku hiyo na anakumbuka huzuni kati ya wachezaji wenzake.

"Ilikuwa siku iliyotawala na hisia chungu kwa sababu hatimaye nilikuwa nikitimiza ndoto yangu ya kucheza katika ligi kuu nikiwa na kikosi cha kwanza na kufikia yote ambayo nimewahi kutaka kwa bahati mbaya tukashuka daraja,"

"Lakini kwa upande mwingine hayakuwa matokeo tuliyotaka na hadi mwisho wa mechi ilikuwa giza sana kwa upande wetu." amesema Melamad.