
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP), Simon Sirro
IGP Sirro amesema hayo leo Novemba 19, 2021, akiwa Mkomazi mkoani Tanga, wakati alipofanya ziara ya ukaguzi kwenye eneo la kambi ya mafunzo ya medani za kivita ambapo zaidi ya askari 700 wa cheo cha Mkaguzi wa Polisi wanapatiwa mafunzo ya medani kwenye eneo hilo.
Aidha, IGP Sirro amesema kuwa katika kuelekea kwenye miaka 60 ya Uhuru, Jeshi la Polisi limejipanga kuhakikisha amani na utulivu inazidi kuimarika nchini na kuwataka wananchi kuendelea kutoa ushirikiano kwa jeshi hilo ili kufichua uhalifu na wahalifu na wale watakaojaribu kuvuruga amani ya nchi wataendelea kushughulikiwa kwa mujibu wa sheria.