Sunday , 26th Dec , 2021

Aliyekuwa Askofu Mkuu wa Kanisa la TAG Tanzania Askofu Prof. Ranwell Mwenisongole amefariki dunia. Askofu Prof. Mwenisongole alikuwa Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la City Christian Center (CCC)- TAG Upanga Jijini Dar es Salaam na alikuwa Askofu Mkuu Mstaafu wa TAG Tanzania kwa Awamu ya Pili

Aliyekuwa Askofu Mkuu wa Kanisa la TAG Tanzania Askofu Prof. Ranwell Mwenisongole

Ofisi ya TAG Makao Makuu Dodoma imethibitidha na kueleza kuwa Askofu Mwenisongole alikuwa akisumbuliwa na maradhi ya Kisukari na Shinikizo la Damu.