
Chelsea iliomba mchezo wao na Wolves mnamo Disemba 19 uahirishwe, lakini Shirikisho la kandanda nchini humo ilikataa ombi hilo.
Wakati mechi 15 za EPL zikiwa zimeahirishwa hadi sasa mwezi Disemba, Chelsea walikuwa wakicheza mechi yao ya nane katika mashindano yote katika mwezi huo na wanakibarua dhidi ya Brighton kutika dimba la Stamford Bridge siku ya Jumatano.
Tuchel ameiomba FA ya Uingereza kurudisha idadi ya wachezaji wa akiba wanaoweza kucheza kuwa tano, ilikuweza kulinda wachezaji wao dhidi ya majeruhi na kuweza kudhibiti ufinyu wa kikosi kutokana na mlipuko wa UVIKO-19 kwenye kambi za timu mbali mbali za EPL.