Monday , 3rd Jan , 2022

Baada ya kutapakaa kwa tetesi za kiungo wa Yanga, Mukoko Tonombe wa Yanga kudaiwa kugomea mkataba mpya wa klabu ya Yanga, wadau wengi wa timu hiyo walimwona kama anafanya usaliti.

Tonombe alisema hajagomea mkataba mpya, lakini bado hajafuatwa na uongozi wa Yanga ili kujadili juu ya kuongeza ili aendelee kusalia klabuni hapo.

“Sijagoma kuongeza mkataba mpya, ila ukweli hadi sasa sijafuatwa juu ya kuongeza, ila mjue mi bado ni mchezaji wa Yanga kwani nina mkataba uliosaliwa na miezi sita,” alisema Tonombe.

Raia uyo wa DR Congo alisema suala la kuongeza mkataba litakuwa na kipaumbele kikubwa cha yeye kucheza kwa sababu hilo ndio jambo kubwa anatarajia kuliona ili aendelee kuwepo kwenye timu ya Taifa.

Akizungumzia kuhusu kuhusishwa kuwa yupo mbioni kujiunga na RS Berkane pamoja na Simba, Mukoko alisema; “Hapana! Mi bado ni mchezaji wa Yanga hizo ni tetesi tu kama zingine.”

Tonombe kwenye msimu uliopita alikuwa ni mchezaji tegemeo kwenye kikosi cha Yanga katika eneo la kiungo akicheza sambamba na Feisal Salum ambaye sasa anacheza kama mshambuliaji wa pili (Namba 10).

Msimu huu Mukoko hapati nafasi ya kuanza kwenye kikosi cha kwanza baada ya kusajiliwa Khalid Aucho na Yanick Bangala ambao wameonyesha pacha nzuri tangu waanze kucheza.