(Mcheza Tennis wa China, Peng Shuai)
Peng alichapisha andiko lenye maneno 1600 Novemba2, 2021 katika ukurasa wake wa wa mtandao wa Weibo akimshutumu kiongozi wa ngazi ya juu wa zamani wa serikali ya China, Zhang Gaoli kwamba alikuwa anamlazimisha kuingia kwenye mahusiano ya kimapenzi bila ya ridhaa yake, andiko ambalo alilifuta muda mchache baadaye.
Na baada ya Peng kuandika tuhuma hizo hakuonekana kabisa kwa muda wa wiki kadhaa na kuleta hali ya sintofahamu katika jamii ya wanamichezo duniani.
Hii sasa ni mara ya pili Peng kufanya mahojiano na kukanusha tuhuma hizo akisema watu wengi walielewa vibaya kuhusu chapisho lake hilo na hakuna haja ya kuzidi kulizungumzia tena jambo hilo, huku wadau wengi wakichukulia kanusho hili kama propaganda ya kulimaliza sakata hilo.

