Nyota wa tennis Daniil Medvedev
Medvedev mwenye umri wa miaka 26, alimuondoa Mjapan Yoshihito Nishioka kwa seti 2-0 ( 6-2 6-3) huku jumatatu nyota huyo akitarajiwa kushika nafasi ya kwanza kwa viwango vya ubora duniani baada ya nyota raia kutoka Serbia Novak Djokovic kuondolewa ambaye alipoteza mbele ya raia wa Czech Jiri Vesely mjini Dubai.
"sio rahisi kucheza mchezo huku ukipokea taarifa nzuri za kwenda kuwa nafasi ya kwanza kwa ubora duniani ingawaje lengo la kwanza ilikuwa kushinda kwa kila mchezo na kufanya vizuri"amesema Medvedev
Upande wa Nadal mwenye umri wa miaka 35 ambaye alitwaa taji la Grand Slam la 21 mjini Melbourne yeye alitinga hatua ya nusu fainali baada ya kumfunga Muingereza Tommy Paul kwa seti 6-0, 7-6 (7-5) huku nusu fainali ya pili itawakutanisha Muingereza Cameron Norrie atakayecheza na Mgiriki Stefanos Tsitsipas.



