Sunday , 27th Feb , 2022

Aliyekua kocha mkuu wa Leeds United Marcelo Bielsa ametimuliwa kazi na klabu ya Leeds United baada ya kua mwenendo wa matokeo mabaya baada ya timu hiyo kukosa ushindi katika michezo sita mfululizo na kufungwa michezo minne mfululizo kwa idadi kubwa ya magoli.

(Kocha Marcelo Bielsa)

Muargentina huyo mwenye umri wa miaka 66, alipewa kibarua hicho mwezi Juni mwaka 2018, anaondoka akiwaacha Leeds wakiwa na tofauti ya alama mbili tu juu ya eneo la kushuka daraja. Chini ya Bielsa, Leeds walimaliza katika nafasi ya tisa msimu uliopita, ambao ndio walirejea Ligi Kuu ya England baada ya kukosekana kwenye ligi hiyo kwa takriban miaka 16.

Lakini kipigo cha magoli 4- 0 cha Jumamosi hii kutoka kwa Tottenham kiliwafanya kupoteza mechi zao nne zilizopita kwa kufungwa jumla ya mabao 17 kwa 2.

Walipokua katika ligi ya championship Leeds walikuwa wakimaliza katika nafasi za katikati ya msimamo katika misimu sita kati ya saba waliyocheza katika ligi hiyo daraja la kwanza kabla ya kuwasili kwa Bielsa na kuchukua mikoba ya kuinoa timu hiyo. Baada ya kuwachapa Derby country katika mechi ya mchujo kwa msimu wa 2018-19, Leeds united chini ya Bielsa ilipandishwa daraja wakiwa mabingwa wa champioship mwezi Julai mwaka 2020.