Gwiji wa zamani wa soka Pele
Pele mwenye umri wa miaka 81, ambaye ni bingwa mara tatu wa kombe la dunia alilazwa mjini Sao Paulo ambapo kwenye taarifa waliyoitoa hospitali ya Albert Einstein alipolazwa Pele imesema "hali yake imeimarika na tatizo la UTI amepona ingawaje bado ataendelea kuja hospitali kwa ajili uangalizi hasa oparesheni aliyofanyiwa ya utumbo mpana”.
Mwaka 2014, Pele alilazwa hospitali kwa tatizo la UTI na kupelekea kufanyiwa uchunguzi wa figo yake huku figo ya kulia ilitolewa mwaka 1970 kutokana na majeraha aliyoyapata akiwa mchezaji huku 2019 akifanyiwa upasuaji wa kuondolewa mawe kwenye figo yake.
Pele ambaye anaheshimika kama miongoni mwa wachezaji bora kuwahi kutokea duniani kwenye kandanda, ndani ya timu ya taifa ya Brazil “Selecao” anaongoza kwa ufungaji wa magoli akifunga mabao 77 kwenye michezo 92.



