Wednesday , 2nd Mar , 2022

Msemaji Mkuu wa serikali Gerson Msigwa, amesema kwamba serikali haijalipia kuweka tangazo la Tanzania katika jengo refu kuliko yote duniani la Burj Khalifa lililopo Dubai, bali limewekwa kuitangaza nchi kutokana na uhusiano mzuri uliopo na Umoja wa Falme za Kiarabu.

Kushoto ni picha ya Rais Samia iliyowekwa kwenye jengo la Burj Khalifa na kulia nai Msemaji Mkuu wa Serikali Gerson Msigwa.

Taarifa hiyo ameitoa hii leo Machi 2, 2022, kupitia ukurasa wake wa Twitter na kusema kuwa utawala wa Dubai umeweka tangazo hilo kwa kutambua ziara ambayo Rais Samia Suluhu Hassan, aliyoifanya Dubai na utawala huo umeahidi kuendelea kuitangaza Tanzania kupitia jengo hilo maarufu.