Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira Dkt. Selemani Jafo.
Dkt. Jafo ameyasema hayo leo Machi 2, 2022, Jijini Dodoma kuelekea mwaka mmoja wa uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan, ambapo amesema katika kuonesha jitihada hizo tayari wameanza kushauriana na wahusika ili kufanikisha jambo hilo kwani kwa kufanya hivyo watakuwa wametunza mazingira na kutunza afya za wananchi.
Katika hatua nyingine Waziri Dkt. Jafo, ameagiza wamiliki wa kampuni kuhakikisha kabla hawajaanza uzalishaji wa bidhaa zao wawe wamepatiwa cheti cha utunzaji wa mazingira kutoka wizara husika lengo ni kuhakikisha kila mfanyabiashara na mwekezaji anatunza mazingira.


