(Mbio za Langa langa za Urusi msimu uliopita)
Mbio hizo zilizokua zimepangwa kufanyika mwezi Septemba mwaka huu katika jiji la St Petersburg, Sasa hazitafanyika tena na uamuzi huo unamaanisha Formula 1 haitashirikiana na Urusi katika mchezo huo kwa siku zijazo, na taarifa inasema kwamba wanaweza kusimamisha kwa muda mrefu zaidi kama Rais Putin ataendelea kubaki madarakani.
(Bingwa wa Dunia wa Formula 1 Max Verstappen)
Naye Bingwa wa dunia wa formular 1 Max Verstappen ametia saini mkataba mpya na kampuni ya Red Bull utakaodumu hadi mwisho wa mwaka 2028, mkataba wenye thamani kati ya paund million 33.3 na paund million 41.7 kwa mwaka, ambao unatajwa kua ni moja kati ya mikataba mikubwa yenye tahamni kubwa zaidi katika historia ya Formula1.









