Friday , 29th Apr , 2022

Bodi ya juu ya maamuzi ya chama cha kikomunist  nchini China, imesema kuwa serikali ya nchi hiyo itachukua hatua ili kuuinua uchumi wa  nchi hiyo kutokana na tishio la janga la Uviko - 19 na vita vinavyoendelea nchini ukraine  kutishia ukuaji wa uchumi wa nchi  hiyo . 

Bodi hiyo iliyokutana leo chini ya Rais Xi Jinping  imesema kuwa serikali itaweka maazimio ya kuboresha viwanda na wafanyabiashara wadogo walioathirika na majanga hayo, huku nchi hiyo ikiwa kwenye karantini na kuathiri uzalishaji.

Taarifa kutoka kwenye mkutano wa chama hicho imesema kuwa janga la Uviko - 19 na vita vya Ukraine vimesababisha changamoto kubwa  na kwamba hatua za makusudi zitachukuliwa ili kulinda uzalishaji, ajira na mfumuko wa bei ili kuboresha maisha ya wananchi.
 
Beijing imejiwekea malengo ya ukuaji uchumi kwa kiwango cha asilimia  5.5 mwaka huu, lakini wataalamu wa uchumi wanaamini kuwa kiwango  hicho huenda kisifikiwe.