Tuesday , 3rd May , 2022

Kiungo mshambuliaji wa Manchester United raia wa Ureno Bruno Fernandes amefikisha mabao 50 akiwa na klabu hiyo, baada ya kufunga bao 1 kwenye mchezo wa Ligi Kuu walioshindi mabao 3-0 dhidi ya Brentford jana Usiku katika dimba la Old Traford.

Bruno Fernades

Katika ushindi huo Bruno alifunga bao la kwanza dakika ya 9 ya mchezo huo, hili ni bao lake la 10 msimu huu kwenye Ligi Kuu England na michuano yote katika michezo 44 na ni bao lake la 50 akiwa na kikosi cha The Red Devils. Magoli mengine kwenye ushindi huo yamefungwa na Cristiano Ronaldo na Rafael Varane.

Bruno alijiunga na Manchester United katika dirisha dogo la usajili la mwezi Januari mwaka 2020 ukiwa ni msimu wa 2019-20 akitokea Sporting Lisbon ya Ureno katika msimu huo alifunga mabao 12 kwenye michuano yote katika michezo 22. Na msimu uliofuata wa 2020-21 alifunga mabao 28 kwenye michuano yote katika michezo 58 na mabao 18 alifunga kwenye michezo ya Ligi Kuu England EPL.

Kwa ujumla amehusia kweye mabao 89 tangu ajiunge na klabu hiyo kutoka jiji la Manchester mabao 50 lakini pia ametoapasi za kufunga mabao (Assists) 39 katika michezo 124.

Tangu Bruno Fernandes ajiunge na Manchester United ni Mohamed Salah wa Liverpool aliyehusika kwenye mabao 73 na Harry Kane wa Tottenhma aliyehusika kwenye mabao 65 ndio waliomzidi kwenye orodha ya wacheazji waliohusika kwenye mabao mengi ya Ligi Kuu England EPL kiungo huyo amehusika kwenye mabao 61.