Thursday , 12th May , 2022

Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Sanaa na Utamaduni, Dk Hassan Abbas amesema filamu ya Royal Tour itaendelea kutoka kwa awamu kwa sababu yapo maudhui mengi ambayo hayapo katika filamu inayiosambaa kwa sasa duniani.

Akizungumza Ikulu ya Dar es salaam kuhusu masuala mbalimbali yaliyojitokeza katika ziara mbalimbali za Rais Samia Dk Abbas amesema kuwa kila baada ya muda watafanya tathmini kabla ya kuachia maudhui mengine ya filamu hiyo.

"Royal Tour ya Tanzania iliyorekodiwa ile inayosambaa duniani ina dakika 57, lakini kuna Material kwa ujumla ambayo yahajatumika ya zaidi ya saa 40 tunayo, kwahiyo huku mbele kila baada ya muda tutakuwa tunatoa toleo jingine" ameeleza Dk Abbas.

Akizungumzia maendeleo ya filamu hiyo amesema nchini Marekani kwa sasa zaidi ya Televisheni 300 zinaonyesha filamu hiyo na muitikio ni mzuri.

"Royal Tour tunakaribia Televisheni  300 katika zile 350 nchini Marekani zinazoendelea kuonyesha, na kila Televisheni  inayoonyesha taarifa ni kwamba kiwango cha wanaoangalia ni kikubwa kuliko Royal Tour nyingi sana" - Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Sanaa na Utamaduni, Dk @Abbastz2