Saturday , 21st May , 2022

Kylian Mbappe ameamua kusalia katika Klabu ya PSG na kuhitimisha taarifa ya kutimkia Real Madrid huku vyanzo vikiripoti kuwa atasaini Mkataba wa miaka mitatu na wababe hao wa soka nchini Ufaransa.

Kylian Mbappe akishangilia bao

Raia huyo wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 23 amekuwa gumzo katika kipindi hiki ambacho Mkataba wake na PSG unaelekea ukingoni huku Real Madrid ndiyo timu iliyokuwa ikipewa nafasi ya kumsajili kinda huyo.

Mbappe atasaini Mkataba mpya utakaomuwezesha kupokea kitita cha paundi Milioni 100 kama fedha ya usajili huku akiwa ni sehemu ya kupendekeza ni wachezaji gani wasajiliwe katika kikosi cha PSG pamoja na Kocha Mkuu.

Mkataba wa Mbappe na PSG utamalizika Juni 30,2022 na inadaiwa atasaini mpya utakaomuweka Parc de Princes hadi 2025.