Monday , 23rd May , 2022

Baadhi ya wabunge wameonyesha hisia zao kwa vitendo  baada yakutoridhika na utekelezaji wa ahadi za serikali zinazotolewa katika majimbo yao kutokana na sababu mbalimbali kutoka Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi.

Wakichangia hotuba ya Bajeti ya Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi kwa Mwaka wa fedha 2022/2023 iliyoomba Trilioni 3.866 ambapo wabunge hao kwa nyakati tofauti walionyesha hisia zao kwa kuangua kilio na kupiga sarakasi ndani ya Bunge hali iliyopelekea Spika wa Bunge kuingilia kati kwakuwataka watendaji wa serikali kufanyia kazi maombi mbalimbali yanayotolewa na wananchi.

https://youtu.be/q-L1sIhrl8g

Mbunge wa Ukonga Jerry Silaa alijikuta akiangua kilio Bungeni huku Mbunge wa Mbulu Vijijini Flatei Massay akiamua kupiga sarakasi kama ishara ya kutoridhishwa na ahadi za barabara jimboni kwake

Katika hatua nyingine Spika wa Bunge Dk.Tulia Anson amewataka Mawaziri na Manaibu Mawaziri kuwa na uhakika wa majibu wanayoyatoa kwakua mara kadhaa baadhi yao wamekua wakitoa majibu yenye utata.