
Kikosi cha Polisi Tanzania
Polisi Tanzania ilitoa mapumziko ya siku saba kwa wachezaji wake baada ya kumalizika kwa michezo dhidi ya Mtibwa Sugar na Biashara United na kupisha kalenda ya michuano ya kimataifa kufuzu kwa michuano ya Afcon 2023 inayotarajiwa kufanyika nchini Ivory Coast
“tumeanza mazoezi leo kutokana na umuhimu wa kutafuta alama kwenye michezo miwili na tumeamua kuweka hapa kambi kwa kuwa hali hewa ya hapa haitofautiani na ya Lindi na ni sehemu tulivu kwa ajili ya kambi “imesema taarifa kwa umma iliyotolewa na klabu hiyo leo.
Polisi Tanzania inashika nafasi ya 7 katika msimamo wa ligi kuu ya NBC ikiwa imejikusanyia alama 33 baada ya kucheza michezo 26 ikiwa imesaliwa na michezo 4 dhidi ya Namungo, Yanga, Geita na Kagera huku Juni 16 ikitarajiwa kupambana na Namungo katika uwanja wa Ilulu