Wednesday , 15th Jun , 2022

Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) kwa ushirikiano na Ofisi ya Takwimu ya Korea Kusini, watapatiwa mafunzo ya kujengewa uwezo, kupatiwa Kompyuta 50, Vishikwambi 10,000 na kuimarishiwa maabara ya habari ya ofisi hiyo, msaada ambao umeelezwa kurahisisha zoezi la Sensa ya Watu na Makazi 2022.

Mtakwimu Mkuu wa serikali ya Tanzania Dkt.Albina Chuwa, na Meneja Mradi kutoka Ofisi ya Takwimu ya Korea Kusini ,Charlie Seo, wakisaini mikataba hiyo

Makubaliano hayo yamesainiwa mkoani Iringa na Mtakwimu Mkuu wa serikali ya Tanzania Dkt.Albina Chuwa, na Meneja Mradi kutoka Ofisi ya Takwimu ya Korea Kusini ,Charlie Seo kwenye mafunzo kwa walimu wa Sensa ya Watu na Makazi ya 2022.

Kwa kupitia ushirikiano huo NBS watapatiwa mafunzo katika nyanja mbalimbali ndani ya nchi na nchi ya Korea Kusini.