
Timu ya Taifa ya Walemavu ( Tembo Worriors) leo Juni 16,2022 imekaribishwa katika Bunge
Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Mohamed Mchengerwa amewasilisha salamu za pongezi kwa Tembo Worriors mbele ya Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt.Tulia Akson ndani ya Ukumbi wa Bunge leo Juni 16, 2022 Dodoma.
Wachezaji hao wameitwa bungeni kufuatia kufuzu kushiriki Michuano ya Kombe la Dunia kwa Walemavu inayotarajiwa kufanyia Oktoba mwaka huu nchini Uturuki.
Inakuwa mara ya pili kwa kanuni kutenguliwa na timu ya Taifa kupewa nafasi ya kuingia ndani ya Bunge ambapo hivi karibuni timu ya Taifa ya Wanawake U17 Serengeti Girl ilipewa nafasi kama hiyo.
Wakiongozwa na mpambe wa Bunge wachezaji hao waliingia bungeni na Wabunge kuanza kuwashangilia.