Error message

  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 664 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 675 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 679 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).

Ujenzi wa ofisi ya msajili wa vyama vya siasa

Thursday , 23rd Jun , 2022

Naibu Katibu Mkuu  Ofisi ya Waziri Mkuu  anayeshughulikia Sera, Bunge na Uratibu Bwa. Kaspar Mmuya amepongeza maendeleo ya ujenzi wa ofisi  za  msajili wa vyama vya siasa  nchini zinazojengwa eneo la Kilimani  Jijini Dodoma zitakazogharimu  zaidi ya shilingi bilioni 20.

Naibu Katibu Mkuu huyo aliyasema hayo alipofanya ziara ya kutembelea  na  kukagua ujenzi huo unaofanywa na kampuni kutoka China ya Group Six International Limited ukisimamiwa na  mshauri kutoka Chuo Kikuu cha Ardhi.

Alisema ujenzi  unatarajiwa kukamilika baada ya miezi 12 akisisitiza kuongezwa kwa rasilimali watu, muda wa kazi pamoja na vifaa ili kufanya kazi ndani ya muda uliopangwa.

“Niwapongeze kwa kazi kubwa ambayo mnaifanya Ofisi ya Msajili wa vyama vya sisisa  kwa usmamizi mkubwa mnaoufanya lakini endeleeni kuongeza umahiri na kuwasaidia wenzetu wa Group Six  International wafanye kwa matokeo zaidi,” alisema Naibu Katibu Mkuu huyo.

 Pia aliamuagiza mshauri wa ujenzi kufika mara kwa mara katika eneo la mradi  na kufanya kazi kwa kushirikiana na watendaji wengine  kufahamu hali ya ujenzi na kutatua changamoto pindi zinapojitokeza kuhakikisha jengo linajengwa katika hali ya uimara, ubora na usalama.

“Nimshauri mtaalamu wetu awe anatembelea mara kwa mara jengo hili kujionea maendeleo ya kazi kama kuna shida yoyote inatatuliwa  kwa wakati na kufanya marekebisho yanayaotakiwa,”alisisitiza .

Aidha aliwahimiza kuongeza ubunifu wa utendaji kazi kwa kugawa maeneo na muda wa kukamilika kwa kazi kwani itasaidia kuhamasisha kazi kufanyika kwa mwamko na ubora zaidi kama njia ya kuendana na muda wa mkataba unavyotaka.

“Waongeze mtindo wa kufanya kazi kwa kupewa kipande cha kazi kwa muda inasaidia utendaji wa kazi na waangalie ubora usiathiriwe kwa sababu mtu anapopewa eneo lake na muda wa kikomo inamfanya ajitume kwa kasi kubwa,” alieleza Bwa. Mmuya.

HABARI ZAIDI

Baadhi ya Majirani wa Kijana Amani Abed ambaye Amejinyonga baada ya kutoka Hospitali.

Kijana ajinyonga baada ya kutoka hospitali

Antony Blinken, Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani

Marekani yatangaza kulifadhili jeshi la Ukraine

Kaimu Mkurugenzi wa ufuatiliaji na uzingatiaji sheria NEMC,

Wamiliki wa Hospitali nchini wapewa siku 90

Baadhi ya Wakazi wa Kata ya Madanga Mkoani Tanga

Wagoma kubeba mimba kwa kukosa huduma za afya

Mkuu wa mkoa wa Songwe Daniel Chongolo

Wanafunzi 194 washika mimba ndani ya mwezi mmoja

Mabaki ya gari aina ya Noah iliyopata ajali Morogoro

Ajali yachukua uhai wa watu saba Morogoro

Waziri wa Fedha Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba

Wawekezaji wawekeze sekta za uzalishaji - Nchemba

Muonekano wa Kiburugwa ambako Nyumba zaidi ya Tisa Zimebomolewa na Maporomoko ya Tope

Maporomoko ya udongo yasomba nyumba 9 Mbagala