Friday , 8th Jul , 2022

Waziri Mkuu wa zamani wa Japan, Shinzo Abe, aliyekuwa akipatiwa matibabu baada ya kupigwa risasi siku ya leo amefariki dunia. Abe alipigwa risasi wakati akihutubia katika kampeni.

Waziri Mkuu wa zamani wa Japan, Shinzo Abe

Waziri mkuu wa zamani wa Japan Shinzo Abe amefariki dunia baada ya kupigwa risasi mara mbili kwenye hafla ya kampeni ya kisiasa katika mji wa kusini wa Nara asubuhi ya leo Julai 8, 2022.

Maafisa wa usalama katika eneo la tukio walimkabili mshambuliaji huyo, na mshukiwa mwenye umri wa miaka 41 sasa yuko chini ya ulinzi wa polisi.