Error message

  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 664 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 675 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 679 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).

Jela maisha kwa kubaka mtoto wake wa kambo

Wednesday , 10th Aug , 2022

Shabani Budeba maarufu kama Kashenele mwenye  umri wa miaka 60 amehukumiwa kifungo cha maisha na mahakama ya wilaya ya Nyamagana Mkoani Mwanza baada ya kumkuta na hatia ya kumbaka mtoto wake wa kambo mwenye umri wa miaka 12 ambaye ni mwanafunzi wa darasa la nne na kumsababishia Fistula

Kesi hiyo ya ubakaji namba 33 ya mwaka 2022 imesikilizwa  na hakimu Juma Mpuya  na inaelezwa mshtakiwa alitenda kosa hilo kwa nyakati tofauti akiwa nyumbani kwake mwezi Januari na Februaari mwaka huu baada ya mtoto huyo kutoka kwa mama yake eneo la Buhongwa na kwenda wa baba yake wa kambo maeneo ya Mkolani aliko kuwa akiishi na mwanamke mwingine

Maelezo ya upande wa mashtaka  ukiongozwa na wakili wa serikali Gati Mathayo na mwendesha mashtaka Lupyana Mahenge uliokuwa na mashahidi 6 akiwemo muathirika, ambaye alieleza ilipofika usiku akiwa na watoto wenzake mshtakiwa alimwambia akale kwenye nyumba ndogo tofauti na walio lala wenzake ndipo na baadae baba huyo akaingia ndani kumbaka na kitendo hicho kilikuwa kikijirudia 

Mama mzazi wa mtoto huyo alipomfuata aliambiwa na jirani wa familia hiyo kuwa mtoto wake alibakwa baada ya mke wa mshtakiwa kupeleka malalamiko katika serikali ya mtaa ndipo akamuhoji mtoto wake ambaye alikiri na taratibu za polisi na vipimo kufanyika .

Wakati wa kesi mshtakiwa alijitetea mwenyewe na hakuwasilisha shahidi yeyote ambapo alisema hajafanya kitendo hicho na kuhoji siku husika ambazo binti huyo alikaa kwake pia juu ya vipimo kufanyika pasipo kuhusisha mpelelezi wa kesi hiyo.

Kufuatia utetezi huo mahakama imemkuta na hatia na alipoambiwa kujitetea mshtakiwa akasema ana tegemewa na wazazi wake na watoto wake hivyo mahakama impunguzie adhabu

Hakimu Mpuya baada ya kupitia ushahidi wa pande zote mbili alisema mahakama hiyo amesema wakati mshtakiwa anatenda kosa hilo alijua ana wazazi na watotto wanao mtegemea na ametenda kitendo kibaya zaidi ya mnyama hivyo anamuhumu kwenda jela maisha.
 

HABARI ZAIDI

Waziri wa TAMISEMI Mohamed Mchengerwa

Aonya wanaochangia watumishi kutopanda madaraja

Edgar Lungu, Rais wa Zamani Nchini Zambia Akitembea Kuzunguka Mji Mkuu wa Lusaka

Rais wa zamani Zambia Bw. Lungu hatarini kukamatwa

Mkuu wa Ulinzi Ukraine (Picha ya Website)

Zelensky amfukuza kazi mkuu wake wa ulinzi

Baadhi ya Wananchi wa Chindi na Ntinga wakiwa katika Harakati za Kuvuka Mto

Walazimika kulipa hadi 8000 kuvuka mto kwa mtumbwi

Mohamedi Mchengerwa, Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI).

Wanaozuia watumishi kupanda vyeo wakaliwa kooni

Bujukano Mahungu John, Mwenyekiti wa Umoja wa Waganga na Wakunga wa Tiba Asili Tanzania

Waganga wa jadi waungana kukemea ukatili, Geita

Mhe. Kassim Majaliwa, Waziri Mkuu wa Tanzania

Mvua zilizoambatana na upepo zimeua watu watano TZ

Muonekano wa Eneo la Somanga baada ya Mawasiliano kati ya Lindi na Dar es Salaam kurejeshwa.

Mawasiliano yarejeshwa barabara ya Dar - Lindi

Naibu Waziri wa Nishati, Judith Kapinga

Kituo cha kupoza umeme kujengwa Tunduma