
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan
Kauli hiyo ameitoa hii leo Agosti 29, 2022, Ikulu ya Chamwino jijini Dodoma, wakati akiwaapisha Majaji pamoja na Kamishna Jenerali wa Magereza.
"Majaji wanawake pamoja na weledi, lakini wanawake wanakua weledi na waadilifu zaidi, dhambi ambazo utazishika kwa Majaji wanaume huzikuti kwa wanawake lakini anahukumu kwa moyo, kama ni mtoto anamuangalia yeye kama mama," amesema Rais Samia
Aidha Rais Samia ameongeza kuwa, "Jaji mwanamme unaletewa mtu amepigwa kachakazwa halafu unamuuliza we kabila gani,anakujibu Mkurya sasa si ndiyo ya kwenu hayo sasa unakuja kufanyaje hapa, na hapo unajisifu umefuata mila na desturi za Tanzania, hapana,".