Monday , 29th Aug , 2022

Mkuu wa wilaya ya Handeni Sirieli Mchembe ameomba msaada wa haraka kutoka mamlaka ya hifadhi ya wanyama pori TAWA kuwanusuru wananchi na tembo zaidi ya 50 waliovamia maeneo yao

Tembo hao wamevamia maeneo hayo na kuharibu mimea huku wakijeruhi wananchi katika vijiji vya Kwamatuku, Komsala, Mbagwi na Mzeri wilayani humo

Kufuatia tembo hao wananchi wa vijiji hivyowamelazimika kuyahama makazi yao

Tembo hao wanadaiwa kutokea hifadhi ya Mkoamazi iliyopo katika wilaya ya Same mkoa wa Kilimanjaro na wamedaiwa kuvamia maeneo hayo mara kwa mara na kusababisha vifo na uharibufu wa mazao ya wananchi shambani