
Vijana wanufaika wa mkopo wa halmashauri
Nchini Tanzania sera ya vijana inaendelea kutekelezwa kwa vitendo, mathalani katika mamlaka za halmashauri zote, kumeelekezwa kwamba 10% ya mapato ya ndani itumike kutoa mikopo kwa vijana. Katika kutekeleza matakwa hayo ya kisera, tayari vijana idadi nane wamenufaika na mkopo wa Mil. 110 kutoka halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam ambayo wameitumia kujenga zahanati katika eneo ambalo hakukua na huduma ya afya Jijini hapa.
“Kwanza haikuwa rahisi kufungua hii zahanati kwasababu tulitumia miaka miwili kupata mkopo huo ambao tumeutumia kijenga hii zahanati, tulijikusanya tukawaza na tukaona tuandike and iko la kuomba kupewa pesa kwa ajili ya mradi huu. Tunaishukuru serikali kwakweli ikatusaidia kupata hizi fedha, na tulipozipata hatukuwaza kugawana. Kwahiyo ni sehemu ya 10% ya mapato ya ndani ya halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam”- Sefania Mwanja – Mganga Mfawidhi, Zahanati ya Afya ya Jamii.
Hatahivyo, inaelezwa kuwa hakukuwepo na kituo cha huduma ya afya katika meneo haya hapo awali, wakazi wa viunga vya Kipunguni wamesema namna ambavyo zahanati hii itaenda kuwasaidia kwani hawatatumia tena gharama kubwa kutafuta huduma hii mhimu.
“Kwakweli sisi hapa tulikuwa tunategenea kwenda Pugu, FFU au Amana kupata huduma ya afya, ilikuwa si tu inatoboa mifuko yetu kwasababu ya gharama kubwa... bali ilikuwa ni hatari kwa maisha kwasababu ya hali ya usafiri wa Jijj hili hasa usiku. Kwahiyo hata kliniki tu ilikuwa inatulazimu kutembea umbali mrefu sana au kupanda pikipiki ambayo ni gharama kubwa na hatari kwa wajawazito ili kupata huduma"- Janeth Mwise – Mkazi wa Mtaa wa Amani, Kipunguni.