Wednesday , 28th Sep , 2022

Balozi wa Tanzania nchini Saudi Ali Jabir Mwadini amesema mpaka sasa hakuna mfanyakazi wa kazi za ndani kutoka Tanzania aliyepo  nchini Saudi Arabia rasmi 

Balozi Mwadini amesema kwa sasa wanatoa kipaumbele kwa wafanyakazi wenye taaluma zaidi hivyo kesi mbalimbali zinazosikika za waafrika kunyanywaswa Saudi Arabia hazihusishi watanzanii

"Hapa Saudi Arabia mpaka sasa hatuna wafanyakazi wa kike waliokuja kwa njia rasmi, mkazo tumeuelekeza kwa wafanyakazi wenye taaluma kidogo na sio wa majumbani, kama mnasikia kesi za wafanyakazi wa majumbani itakuwa ni raia wa Burundi, Uganda, Ethiopia na Kenya"

Balozi Mwadini ametoa taarifa hiyo katika mkutano wake kwa njia ya mtandao (Zoom) 

Aidha Balozi Mwadini amewataka watanzania kuchangamkia fursa zinazopatikana nchini Saudi Arabia huku akisisitiza vipo baadhi ya vitu vinavyodharauliwa Tanzania lakini ni biashara

"Kuna vitu duniani ni mali lakini Tanzania havitumiki , kwa mfano kwenye Nazi kifuu cha Nazi ndio sehemu yenye bei kuliko sehemu yotote ya Nazi, lakini huko Tanzania wanatupa, ni mali sana katika uzalishaji wa mazao mbalimbali, inasaidia kutunza maji"

"Zipo biashara nyingi za kuuza hapa Saudi Arabia kama Samaki na mazao mengine ya baharini, Nyama na bahati nzuri sana miongoni mwa mambo tuliyofanikiwa ni kufungua tena soko la nyama hapa"

Kuhusu mazomo nchini Saudi Arabia amesema kuwa vyuo vya nchi hiyo ni bora na vinatambulika duniani
"Fursa ipo kwa wasomi, wanaotafuta elimu hapa Saudia Arabia ni sehemu nzuri, na vyuo vya hapa vipo kwenye vyuo bora duniani, wamewekeza vya kutosha katika elimu"