Wednesday , 28th Sep , 2022

Mamilioni ya wakazi wa jimbo la Florida wapo kwenye utayari wa kupokea tukio kubwa linalohatarisha maisha , la ujio wa kimbunga Ian ambacho kitaambatana na upepo mkali na mafuriko makubwa . 

Kimbunga Ian, ambacho tayari kimeshapiga magharibi mwa Cuba kinatarajiwa kuwasili Florida baadae leo.Kimbunga hicho chenye upepo mkali unaofikia kilomita 250 kwa saa ni kibaya kwa mujibu wa mamlaka za hali ya hewa jimboni humo NHC.  

  Inatarajiwa kimbunga hicho kitaelea eneo muhimu jimboni humo, ambapo itakua ni mara ya kwanza kupigwa na kimbunga tangu mwaka 1921 .Kitengo cha uchunguzi wa vimbunga jimboni humo kimesema kwamba eneo la Tampa litapigwa na upepo mkali kuwahi kutokea ndani ya miaka 100 iliyopita , taarifa hiyo ikitolewa na Erik Salna, Mkurugenzi wa kituo hicho .

 Wananchi wamekua wakinunua maji na chakula kama tahadhari huku jumbe zikitumwa kwenye simu zao za kuwataka kuondoka haraka kwenye maeneo hatarishi.