Monday , 3rd Oct , 2022

Wazee nchini wameomba serikali iangalie utaratibu unatumika na mpango wa kunusuru kaya maskini TASAF ili kuingiza wazee wengi  wasio na uwezo wapate fedha za kujikimu.

Mwenyekiti wa Baraza la Wazee, Mzee Lameck Sendo

Akizungumza kwa niaba ya wazee nchini ikiwa leo Tanzania imeadhimisha siku ya wazee Mwenyekiti wa Baraza la Wazee, Mzee Lameck Sendo amesema bado kundi hilo linakutana changamoto mbalimbali ikiwa ni pamoja na ukatili kwa wazee, kuuwawa kwa imani potofu na kukosa huduma za afya huku wakiomba serikali kumalizia mchakato wa sera ya taifa ya wazee ya mwaka 2003 ili kuwasaidia katika upatikanaji wa haki zao za msingi.

Akijibu changamoto kwa niaba ya Waziri Mkuu Mhe.Kassim Majaliwa ,Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Uratibu na Bunge Mhe.George Simbachawene ameitaka jamii kuacha kuua wazee na kuwanyanyapaa huku akisisitiza serikali inatatua changamoto zinazowakumba wazee ili wapate haki zao za msingi kama binadamu wengine huku akiagiza vyombo vya dola kuchukua hatua kazi dhidi ya wahalifu wa mauaji.