Friday , 7th Oct , 2022

Mkuu wa Mkoa wa Geita Martine Shigella ametoa ahadi ya kutoa viwanja bure  kwa wawekezaji watakaowekeza katika halmashauri yeyote mkoani humo ili kuvutia wawekezaji wengi kutoka maeneo mbalimbali ndani na nje ya nchi kwa ajili ya kuboresha rasilimali zipatikanazo mkoani humo

Shigela ameyasema hayo kwenye maadhimisho ya siku ya Geita yenye lengo la kutangaza fursa za uwekezaji kwenye sekta ya kilimo, uvuvi, ufugaji na biashara zinazopatikana mkoani humo.

"Nazielekeza halmashauri katika miji mipya, katika maeneo mapya ukitaka uwekezi mwananchi na mfanyabiashara anatafuta wapi kuna good environment nafarijika kuwatangazia halmashauri ya mji wetu wa Geita na baadhi ya halmashauri ndani ya mkoa  wa Geita tuko tayari kutoa ardhi bure kwa muwekezaji anaetaka kuja kuwekeza na tumejiwekea malengo ukija watu 10 wa kwanza wakaja na mpango wakaja na fedha wakatuambia ndani ya mwaka  mmoja tutalipa title tusaini makubaliano nitajenga hotel ya nyota tatu nyota nne, nitajenga kiwanda chenye kuprocess mazao nyatokanayo na wakulima wetu tunakupa Ardhi bure", alisema Shigela. 

Kwa upande wake Katibu tawala mkoa wa Geita Godius Kahyarara ameutangaza mradi mpya wa kilimo cha Kisasa  wa Ibanda ambao umeanzishwa kwa ajili ya kukuza sekta ya kilimo mkoani humo.

"Ibanda industrial park within the same area, mtanisahihisha kwa sababu tukienda kwenye maeneo ya viwanda kule Pugu hatuwezi kukuta mkono wa kushoto kuna viwanda alafu kulia  kuna mashamba, kwa hivyo ni vitu vyote ambavyo tumevizingatia katika kutengeneza huu mradi wetu, tutakapokuwa tumeendeleza huumradi wetu unahitaji viwanda", alisema Kahyarara. 

Mkurugenzi wa halmashauri ya mji Geita Zahra Michuzi anasema serikali kupitia wizara ya kilimo imewapatia shilingi bilioni 6.5  kwa ajili ya uboreshaji miundombinu na uanzishwaji wa mradi huo ili uweze kuleta tija kwa wananchi.

"Eneo hili lipo katika sura mbili, sura ya kwanza ni industrial park na sura ya pili ni agricultural park, katika mradi wetu huu wa agricultural park tayari wizara ya kilimo imetupatia shilingi bilioni 6.5 kuhakikisha kwamba eneo hili tunaenda kulitumia ipasavyo na kuleta tija katika halmashauri ya mji, mkoa wa Geita na taifa kwa ujumla, tumeweza kuonana na wenzetu wa SUA, ambao wapo katika mchakato wa kutuandikia andiko la cha nini kifanyike pale na hii tija ndio tunaitaka inatokea na kuleta mabadiliko ya kiuchumi', alisema Michuzi.