Wednesday , 12th Oct , 2022

Moto mkubwa umeteketeza bidhaa pamoja na vibanda vya wafanyabiashara zaidi ya 200 wa soko la Ruaha Mikumi mkoani Morogoro.

Moto soko la Ruaha

Mwenyekiti wa soko hilo, Ebu Lipenege amesema mbali ya bidhaa kuungua, pia baadhi ya wafanyabiasha wameibiwa bidhaa zao na watu waliokuwa wakivunja maduka na kuondoka na bidhaa.

Mwenyekiti huyo amesema kuwa soko hilo lilianza kuungua moto saa 3 usiku, Oktoba 10 lakini haikuwezekana kuuzima kutokana na udhaifu wa vifaa vya kuzimia moto, huku gari la Zima moto likishindwa kufika kwenye chanzo cha moto.

Kwa upande wake Diwani wa kata Ruaha, Alex Gwila amewataka wafanyabiasha hao kuwa na moyo wa subira na uvumilivu wakati wataalamu wakiendelea kuchunguza tukio hilo.

Kufuatia tukio hilo Mkuu wa Wilaya ya Kilosa, Alhaji Majid Mwanga ameunda kamati maalumu inayowajumuisha wataalamu kutoka jeshi la zima moto na jeshi la Polisi kuchunguza tukio hilo ili kujua chanzo cha moto na hasara kiasi gani imetokana na moto huo.