
Mkuu wa wilaya ya Nzega, Kamishina Msaidizi wa Polisi Advera Bulimba
Akizungumza wakati akiwasilisha taarifa ya utekelezaji na miradi pamoja na mapokezi ya fedha kwa wilaya hiyo tangu kuingia madarakani kwa Rais Samia Suluhu Hassan, amesema zaidi ya shilingi billion 97 zimepokelewa katika wilaya ya Nzega kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo.
Amesema mpaka sasa wilaya ya Nzega inaendelea na utekelezaji wa miradi ya kimkakati kupitia fedha hiyo katika sekta ya elimu, afya, maji na umeme lengo ikiwa ni kuendelea kuboresha na kusogeza huduma kwa wananchi wa wilaya ya Nzega.