Tuesday , 25th Oct , 2022

Kaimu Katibu Mtendaji wa Baraza  la Mitihani NECTA Athumani Amasi ametangaza kuanza kwa mitihani kujipima ya darasa la nne na kidato cha pili huku  wasimamizi wakitakiwa kufanya kazi zao kwa weledi pamoja na kuwazingitia zaidi watahiniwa wenye mahitaji maalum.

Kaimu Katibu Mtendaji NECTA Athumani Amasi

Amasi akizungumza na waandishi wa habari leo amebainisha mitihani ya darasa la nne inatarajiwa kuanzia Oktoba 26- 27 na kidato cha pili itaanza Oktoba 31 - Novemba 10 huku akibainisha kuongezeka wa idadi ya watahiniwa.

Aidha NECTA wamewaasa walimu wakuu, waratibu elimu kata na wamiliki wa shule kutojihusisha katika kupanga na kutekeleza njama za kufanya udanganyifu katika mitihani hiyo.

Aidha Amasi amewataka wananchi  kutoa ushirikiano wakati wa upimaji huo, hasa watakapo hisi dalili zozote za udanganyifu kwenye mitihani hiyo.