Monday , 31st Oct , 2022

Jeshi la Polisi nchini limekanusha taarifa za upotoshaji zilizodai kuwa Joshua Mkandi wa mkoani Songwe alitekwa na jeshi hilo na badala yake mwanaume huyo alikamatwa na Askari Polisi pamoja na wenzake 12 kwa tuhuma za unyang'anyi wa kutumia silaha na wizi wa pikipiki.

Msemaji wa Jeshi la Polisi nchini SACP David Misime,

Taarifa hiyo imetolewa na Msemaji wa Jeshi la Polisi nchini SACP David Misime, na kusema Askari Polisi waliomkatama Joshua, walikuwa na sare na walijitambulisha kwake.

Joshua na wenzake 12 wanatarajiwa kufikishwa mahakamani hii leo Oktoba 31, 2022 na kuwaomba wananchi kuendelea kuipuuza taarifa hiyo ya upotoshaji iliyosambaa mitandaoni ikieleza mwanaume huyo kutekwa na Jeshi la Polisi.