Wednesday , 2nd Nov , 2022

Serikali imesema kwamba hadi kufikia mwishoni mwa mwezi Desemba mwaka huu tatizo la umeme kukatika litakwisha mara baada ya mradi wa Kinyerezi 1 Extension utakotoa megawati 185 kukamilika.

Naibu Waziri wa Nishati Stephen Byabato

Kauli hiyo imetolewa hii leo Novemba 2, 2022, Bungeni jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Nishati Stephen Byabato, wakati akitoa ufafanuzi kufuatia changamoto ya ukatikaji wa umeme inayoendelea nchini.

"Tunayo changamoto kidogo ya upungufu wa vyanzo vya uzalishaji wa umeme hasa kwenye maji, hilo limepelekea baadhi ya maeneo kukatika umeme au kupewa umeme kwa vipindi tofauti , serikali imeji-commit kabla ya mwezi unaokuja kuisha mradi wetu wa Kinyerezi 1 Extension utakaotupatia megawati 185 umekamilika ili kuondoa matatizo ya kukatika katika umeme," amesema Naibu Waziri Byabato