
Waziri Aweso ameyasema hayo leo, wakati wa kikao chake na taasisi za umma zinazohusika na huduma za maji jijini Dar, ambapo amewataka watumishi wa taasisi hizo zilizo chini ya Wizara ya Maji kushikamana katika kipindi hiki cha mpito na kuhimiza utunzaji wa vyanzo vya maji nchini.
Aidha Aweso amewataka Wakala wa uchimbaji wa visima na mabwawa nchini kuongeza kasi ya kuchimba visima ili kuongeza upatikanaji wa maji katika Mkoa wa Dar es Salaam akiongeza kuwa serikali inatarajia kuchimba mabwawa Dar es Salaam na Dodoma
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi DAWASA na Mkuu wa Majeshi Mstaafu Jenerali Davis Mwamunyange amebainisha kuwa kwa sasa Dar es Salaam inahitaji Maji lita Milioni 544 na kiasi cha Maji yaliyopo ni lita Milioni 520 akisisitiza utunzaji wa vyanzo vya maji.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Ubungo akiahidi kuwa jitihada zinazofanywa na serikali kukabiliana changamoto ya uhaba ya maji katika jiji la Dar es Salaam.