Thursday , 3rd Nov , 2022

Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Geita Safia Jongo, amewatahadharisha wahalifu wanaofanya mauaji na kukimbilia kwenye migodi ya uchimbaji madini kwa kuigiza wao ni wachimbaji kutafuta sehemu nyingine ya kufanyia uhalifu wao lakini sio Geita

Tahadhari hiyo imekuja siku chache baada ya tukio la mauaji ya dereva bodaboda aliyeuawa na majambazi wakati akijaribu kumuokoa mtu mwingine aliyekuwa amevamiwa na majambazi hao

Kamanda Jongo anetembelea baadhi ya migodi mkoani humo  ambayo inasemekana wahalifu wamekuwa wakijificha na kujifanya wao ni wachimbaji 

"Matukio ya wizi, matukio mnajeruhiana, matukio mnauana, matukio mnashambuliana, lakini matukio mengine wengine wahalifu mpo humu, mnaenda mjini mnatupiga mnarudi huku mnajificha, wewe ukijiona unajijua wewe ni muhalifu anza katafuta mahali pa kufanyia uhalifu sio Geita" amesema Kamanda Jongo

"Wewe kama mchimbaji baki endelea na uchimbaji lakini wewe kama umekuja na nia zako tofauti tafuta njia ya kupita Anza mbele", amesema Jongo.

Aidha Jongo amewaomba wananchi kutoa ushirikiano kwa Jeshi la Polisi ili waweze kuwakamata wote wanaohusika na vitendo vya kiharifu mkoani humo.

"Kwahiyo tukishirikiana mimi na ninyi hakuna muhalifu atabaki hapa, haya matukio hqtuwezi kukubaliana nayo, mara mtu kakatwa mkono, mara mtu sijui kafanya nini, mimi sikubali", alisema Jongo.