
Akizungumza na #EATV Kamanda wa Jeshi la polisi Mkoa wa Shinyanga Janeth Magomi, amethibitisha mwalimu huyo kukamatwa ambapo baada ya kufanya vitendo hivyo vya ukatili kwa watoto kuanzia umri wa miaka sita hadi 11 alitoroka na kukimbilia Wilaya ya Kibondo Mkoani Kigoma na walipofuatilia wamemkamata na amerudishwa Kahama kujibu tuhuma zinazomkabili.
Kamanda Magomi amesema Mwalimu huyo aliwarubuni watoto hao kwa kuwapa Sh 1000 na wengine Sh 500 kisha kuwafanyia kitendo hicho ambacho ni kinyume na maadili na kuwataka wazazi na walezi kuwafichuwa watu wanaowafanyia vitendo vya kikatili watoto wao badala ya kuwaficha.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Mtaa wa Shunu Manispaa ya Kahama, Joseph Kaliwa amesema alipata taarifa kutoka kwa wananchi siku ya Ijumaa juu ya kulawitiwa watoto na kushirikisha viongozi wengine ndipo walipoanza kufuatilia na kuandaa kikao cha wazazi ili kupata maelezo ya kina kisha watoto wote walikwenda kufanyiwa uchunguzi hospitali ya Rufaa Kahama na kubaini wameingiliwa.