
Waziri wa Elimu Profesa Adolf Mkenda
Ripoti ya kamati hiyo imesomwa hii leo Novemba 7, 2022, Bungeni jijini Dodoma, na kusema kwamba matokeo hayo pia yamedhihirisha uwepo wa changamoto ya mawasiliano na mahusiano kati ya Wizara ya Elimu na baina ya Wizara na Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu (HESLB).
"Changamoto ya mawasiliano ndani ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imedhihirika kutokana na muda uliotumika kutekeleza maelekezo ya Waziri, Waziri aliunda Kamati hiyo tarehe 12 Julai, 2022 lakini barua za uteuzi kutoka Wizarani zilisainiwa tarehe 31 Agosti, 2022, imechukua takriban mwezi mmoja na nusu kwa uamuzi uliotolewa na Waziri kutekelezwa kwa kuandika Barua," imeeleza ripoti ya kamati ya Bunge
Aidha kamati ya Bunge imehitimisha kwa kusema kwamba serikali inapaswa kutekeleza maagizo ya Bunge, yaliyoelekeza kwamba wanafunzi wote wenye sifa za kupata mikopo na hawajaipata wanapaswa kupokelewa vyuoni wakati serikali ikishughulikia mikopo yao.